Umoja
wa Mataifa umetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu mauaji ya
kikabila dhidi ya raia yaliyofanyika hivi karibuni na kusababisha
mauaji ya mamia ya raia nchini humo.
Umoja
huo wa Mataifa umesema kuwa tukio hilo ni baya kuwahi kutokea katika
nchi hiyo inayokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika
mapambano baina ya majeshi ya Serikali na Waasi.
Waasi
wanaoongozwa na Rieky Machar wanalaumiwa kwa mauaji hayo ingawaje
kiongozi wa waasi hao amesema wapiganaji wake hawastahili kulaumiwa
kutokana na mauaji hayo.
Watu zaidi ya mia moja walipoteza maisha katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Bentui lilioanguka mikononi mwa waasi mwishoni mwa juma lililopita baada ya mapigano na vikosi vya serikali.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire