Bshar al Asad |
Mataifa
11 ya magharibi yakiwemo yale ya jumuiya ya nchi za Kiarabu,
yamemuonya rais wa Syria Bashar al-Asad kuhusu mpango wake wa kufanya
uchaguzi mkuu, kwa kile wanachodai uchaguzi huo hautakuwa huru na
haki.
Kwenye
taarifa yao ya pamoja, nchi zinazojiita marafiki wa Syria wamemtaka
rais Asad kutoandaa uchaguzi wowote wakati huu ambapo hali ya usalama
hairidhishi nchini humo na badala yake kujikita katika mazungumzo ya
kusaka suluhu nchini humo.
Haya
yanajiri wakati huu mataifa Jirani na Syria yakieleza kuzidiwa na
wimbi la wakimbizi wanaokimbia vita huku idadi yao ikielezwa kufikia
zaidi ya milioni moja kwenye nchi ya Lebanon.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire