Mahakama
nchini Senegal itatowa uamuzi hapo kesho kuhusu hatma ya mtoto wa
rais wa zamani wa nchi hiyo Karim Wade anaezuiliwa kwa muda sasa ni
zaidi ya mwaka mmoja kwa tuhuma za kujitajirisha kwa njia zisizokuwa
halali.
Waziri
wa sheria nchini Senegal Sidiki kaba amewaambia wabunge kwamba
Mahakama itatowa uamuzi wake juu ya hatma ya Karim wade na ndipo
itajulikana iwapo kesi itakuwepo au la, kwakuw ajaji anaweza kuamuwa
kuendelea kumzuia ili kuendeleza uchunguzi zaidi.
Karim
Wade alitiwa nguvuni mwa kipindi cha miezi sita tangu April 17 mwaka
2013 jijini Dakar kwa kutuhumiwa kuwa na mali nyingi kinyume cha
sheria, vikiwemo makampuni, ardhi, magari, ambavyo vinakadiriwa kuwa
na thamani ya dola za Marekani Bilioni 1.6.
Karim Wade aliwahikuwa waziri wa utawala bora katika serikali ya baba yake ilioanguka katika uchaguzi mkuu uliomleta madarakani Macky Sall
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire