Bingwa
wa mbio za Olympiki za Marathon upande wa walemavu Oscar Pistorius
ameendelea kupata wakati mgumu mbele ya muendesha mashtaka mkuu
ambaye anahakikisha kuwa utetezi wake kuwa maauaji ya mchumba wake
mwaka uliopita 2013 yalifanyika kwa bahati mbaya, kwamba ni uongo.
Gerrie
Nel ameimbia mahakama kwamba Pistorius alisema uongo kwamba alimuuawa
mpenzi wake Revee Stenkamp kimakosa, na kwamba katika maelezo yake
amekuwa akijikanganya katika muendelezo wa kesi hiyo iliosikilizwa
leo kwa takriban saa moja na nusu kabla ya kuahirishwa wakati
Pistorius alipo jitetea kuwa alihisi kuwa amevamiwa na jambazi kabla
ya kufungua risase.
Bingwa
huyo wa mbio za Paralympiki Oscar Pistorius ameendelea kujitetea
kwamba hakujuwa kwamba ni mpenzi wake katika usiku huo wa siku ya
wapendanao na hivo kufungua mtuto wa bunduki.
Mvutano
huo wa Oscar Pistorisu mwenye umri wa miaka 27 na muendesha mashtaka
ulianza tangu jumatano juma lililopita. Pistorisu ambaye anaendelea
kujitetea kutokuwa na hatia hana haki ya kumuuliza wakili wake katika
hatuwa hii.
Hakuna
anaye tambuwa ni kwa mud gani Garrie Nel ataendelea kupambana na
Oscar kizimbani huku akiendelea kumuhoji maswali yaleyale na
kumtuhumu kuchaguwa maneno na kumtaka akumbue vizuri tukio
lilivokuwa.
Nel
alionekana kuwavutia wengi mahakamani Juma lililopita wakati
alipoonyesha namna gani Pistorius alivyo muuawa mpenzi wake, na
kuonyesha kuwa Pistorius alikusudia kumuuwa mpenzi wake, na kuonyesha
viashiria vya damu zilizoonekana chumbani hapo kabla ya kutokea
mauaji hayo.
Iwapo
itathibitishwa, Pistorius anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela
au miaka 25 Jela.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire