Serikali
ya Kenya imesema itawasajili upya raia wa nchi hiyo kwa mfumo wa
Kieletroniki kama njiamojawapo ya kukabiliana na ukosefu wa usalama
na kuwabaini wageni wanaoishi nchini humo kinyume na sheria .
Usajili
huo utachukua muda wa miezi sita kuanzia mwezi wa sita na wakenya
walio na vitambulisho watarudisha vitambulisho vyao vya zamani ili
kupewa vipya vitakavyowatambulisha kikamilifu.
Polisi
wameendelea kufanya msako jijini Nairobi na mjini Mombasa kuwasaka
wahalifu na watu wanaoishi nchini humo bila vibali.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire