Rwandan musician Kizito Mihigo |
Kundi
la waasi wa kihutu wa Rwanda waliopiga kambi nchini DRCongo FDLR
wamelaani vikali hatuwa ya kukamatwa kwa watu wanaoshukiwa kupanga
njama za kuyumbisha usalama wa Kigali ambao walikamatwa hivi
karibuni.
Katika
taarifa iliotolewa na kanali Willy Irategeka katibu mtendaji wa muda
wa kundi la wapiganaji Abacunguzi, amesema serikali ya Rwanda
imewatia nguvuni wale wote ambao hawataki kuungano na mpango wake
uliokinyume kabisa na demokrasia na hivo kuwatia nguvuni msanii
Kizito Mihigo na muandishi wa habari Cassien pamoja na askari aliye
rejeshwa katika maisha ya kiraia Jean Paul Dukunzeumuremyi.
Serikali
ya Rwanda inasema inaoushahidi kwamba watu hao watatu walikuwa
wamepanga kutekeleza mashambulizi dhidi ya serikali wakishirikiana na
kundi la RNC linalo husiana na Patrick Karegeya, kiongozi wa zamani
wa idara ya ujasusi nchini Rwanda aliauwa mwanzoni mwa kwaka 2014
nchini Afrika Kusini.
Watu
hao wanatuhumiwa pia kushirikiana na kundi la FDLR ambalo wafuasi
wake wanatuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari yaliotekelezwa
nchini Rwanda mwaka 1994.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire