Pages

vendredi 11 avril 2014

OSCAR PISTORIUS AKABILIWA NA WAKATI NGUMU WAKATI AKIHOJIWA NA MUENDESHA MASHTAKA GERRIE NEL

Kesi ya mauaji dhidi ya mwanariadha mwenye ulemavu wa afrika Kusini, Oscar Pistorius, hii leo imeingia kwenye siku yake ya 21 huku upande wa mashtaka ukiendelea kumhoji kwa siku ya 4 mfululizo.

Hii leo mwendesha mashtaka mkuu kwenye kesi hiyo, Gerrie Nel ameendelea kuishawishi mahakama kuwa Pistorius alidanganya kwenye ushahidi wake uliowezesha kupatiwa dhamana na kwamba alidhamiria kumuua mchumba wake, Reeva Steenkamp.

Mara kadhaa Pistorius alionekana kugadhibitshwa na maswali ya mwendesha mashtaka ambaye anadhamiria kuidhihirishia mahakama kuwa mwanariadha huyo alikusudia kumuua mchumba wake kwakuwa hata ushahidi wake unakanganya.

Toka kuanza kuhojiwa na upande wa mashtaka, Oscar Pistorius amejikuta akikiri kuhusika na matukio ambayo awali hakuyaandika kwenye ushahidi wake jambo ambalo linazua maswali iwapo hakudhamiria kumuua mchumba wake.


 Nel huenda akamuhoji Pistorius kwa zaidi ya majuma mawili kabla ya wakili wake Barry Roux kurejea tena kumuuyliza maswali mteja wake.

Kesi ya mwanariadha huyu imeahirishwa hadi siku ya Jumatatu ambapo mwendesha mashtaka, Gerrie Nel ataendelea kumuhoji Oscar Pistorius.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...