Ndege
ya Ufaransa iliyokuwa ikitokea nchini Guinea ambako kumeripotiwa
ugonjwa wa Ebola, imetengwa kwa muda wa saa mbili jijini Paris leo
Ijumaa, baada ya timu ya marubani kuhisi kuwepo kwa abiria mwenye
virusi vya ugonjwa huo hatari, shirika la ndege hiyo limearifu.
Ndege
hiyo imetua kwenye uwanja wa ndege wa Charles
De Gaulle jijini Paris majira ya
asubuhi ikiwa na abiria 187 na timu ya marubani wapatao 11 ambapo
wahudumu wa dharura walifanya ukaguzi kwa wasafiri wote baada ya choo
kichafu kuzusha wasiwasi wa kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola, ambao
miongoni mwa dalili zake ni kuharisha.
Hata
hivyo matokeo ya uchunguzi huo yameonesha kutokuwepo kwa ugonjwa huo
miongoni mwa wasafiri msemaji wa ndege hiyo amesema
Ugonjwa
wa ebola unaweza kuambukizwa kwa binadamu kutoka kwa wanyama wa
msituni na kati ya mtu na mtu kwa njia ya kugusana moja kwa moja kwa
damu,kinyesi ama jasho .
Aidha
kujamiiana na kutohifadhi kwa uangalifu maiti ya mgonjwa wa ebola
pia huweza kusababisha maambukizi.
Mamlaka
nchini Guinea zimeripoti matukio 134 ya ugonjwa wa Ebola tangukuanza
kwa mwaka huu ambapo matukio 86 yamesababisha vifo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire