Polisi
nchini Rwanda imepokonya ardhi ya kituo cha utamaduni wa Ufaransa
kilichofungwa tangu April 16 mwaka huu. Manispa ya jiji la Kigali
iliamuru kufungwa kwa kituo hicho kabla ya kutangazwa kupokonywa.
Balozi wa Ufaransa jijini Kigali Michel Flesch amesema hatuwa hiyo
imechukuliwa kwa tuhuma za kutoheshimu sheria ya mipango miji.
Mea wa
jiji la Kigali Fidele Ndayisaba amefahamisha kuwa hatuwa hiyo
imefuata sheria na ilianza miezi kadhaa iliopita na haina uhusiano
wowote na msuguano wa kidiplomasia ulioshuhdiwa hivi karibuni wakati
wa shewrehe za kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari nchini
Rwanda baina ya mataifa haya mawili.
Balozi
wa Ufaransa nchini Rwanda Michel Flesch amesema manispaa ya jiji
imetaifisha majengo ya kituo cha utamaduni wa Ufaransa na tayari
wamekabidhi kila kitu kwa serikali ya Rwanda. Flesch amesema Manispaa
inasema hawakuheshimu sheria ya Mpango miji.
Balozi
huyo wa Ufaransa jijini Kigali amesema kwa sasa wamesitisha kwa muda
shughuli za kituo hicho wakati huu wakiendelea kulitafutia suluhusu
swala hili.
Kituo
hicho cha Ufaransa kilikuwa kimefungwa tangu mwaka 2006 na 2009 baada
ya uhusinao wa Rwanda na Ufaransa kuwa mbaya, kabla ya kufunguliwa
tena mwaka 2010 baada ya mataifa hayo mawili kutatu tofauti zao.
Mei
wa jiji la Kigali amesema uwanja huo haukuheshimu sheria ya mpango
miji, na kuongeza kuwa amri hii haikuikumba pekee jengo la umaduni wa
Ufaransa, lakini pia majengo mengine.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire