Mbunge
mmoja nchini Somalia amepigwa risase na kupoteza maisha papo hapo
jijini Mogadishu, ikiwa ni siku moja baada ya kuripotiwa mauaji ya
mbunge mwingine wa serikali katika mlipuko wa bomu iliotegwa katika
gari lake, mauaji ambayo yametekelezwa na wanamgambo wa Al Shabab.
Abdiaziz
Isak Mursal ameuawa jumanne karibu na nyumbani kwake katika kata ya
Madina kusini mwa mji mkuu na watu wawili waliokuwa na silaha
waliotimka baada ya kutekeleza mauaji hayo.
Duru
za polisi zimethibitisha kuuawa kwa mbunge huyo aliepigwa risase na
kupoteza maisha papo hapo.
Kundi
la Al Shabab limejigamba kutekeleza shambulio hilo, na lile lilitokea
jana siku ya Jumatatu dhidi ya mbunge Isak Mohamed Ali aliepoteza
maisha huku mwingine Mohamed Abdi akujeruhiwa.
Msemaji
wa kundi la Al Shabab Abdulaziz Abu Musab amesema wao ndio
wanaohusika na matukio hayo dhidi ya wabunge wanaoendesha kazi kwa
faida za wageni na kuwatumia ujumbe mzito wabunge wengine wa serikali
ya Somalia.
Al
Shabab wameahidi kumuawa mbunge mmoja baada ya mwingine.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire