Pages

vendredi 25 avril 2014

KESI YA WATUHUMIWA WA MAPINDUZI KUFUTWA NCHINI SUDANI KUSINI

Waziri wa sheria nchini Sudani Kusini, amefahamisha kuwa ameomba vyombo vya sheria nchini humo kufuta kesi dhidi ya washukiwa wanne wa jaribio la mapinduzi na ambao wanachukuliwa kuwa watu wa karibu na Riek Machar aliyechukuwa uongozi wa uasi tangu mwezi Desemba mwaka jana.

Waziri Paulion Wanawilla amesema ili kutia kipao mbele swala la mazungumzo, maridhiano na uwiano baina ya wananchi wa Sudani Kusini, ameamuru kufuta kesi dhidi ya watuhumiwa hao wanne na ambao wataachiwa huru hii leo.

Kesi dhidi ya watuhumiwa wengine saba walioacha huru na kukabidhiwa serikali ya kenya mwishoni mwa mwezi Januari iliopita nayo pia inatakiwa kufutwa.

Hata hivo, waziri huyo amesema kesi dhidi ya Riek Mashar na watu wake wengine wawili ambo ni Taban Deng Gai gavana wa zamani wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity na Alfred Lado Gore waziri wa zamani wa mazingira na alikuwa mshauri wa rais Salva Kiir ambao ni viongozi waliopambana katika harakati za ukombozi wa taifa hilo na ambo wote wapo mafichoni.

Kesi dhidi ya wajumbe hao wanne ambao ni Pagan Amum katibu mkuu wa chama madarakani cha SPLM, Oyai Deng Ajak waziri wa zamani wa usalama, Ezekiel Lol Gatkuoh balozi wa zamani wa Sudani Kusini jijini Washington, pamoja na Majak D'Agoot naibu waziri wa ulinzi, ilizinduliwa tangu mwezi March iliopita.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...