Akiwa
katika harakati za kutafuta Klabu mpya tangu kuonyesha ishara
iliochukuliwa kuwa ya kibaguzi dhidi ya wayahudi, mshambuliaji wa
Ufaransa Nicolas Anelka ambaye alitajwa hapo awali kuelekea katika
klabu ya Atletico Mineira ya huko Brazil, hatimaye viongozi wa klabu
hiyo wamesema hawataki kumsajili mchezaji huyo kutokana na tabia yake
ambayo sio ya kitaaluma.
Kama
ilivyokuwa ikitarajiwa, Mkurugenzi wa kiufundi wa Klabu ya Atletico
Mineiro Eduardo
Maluf amesema tabia ya nchezaji huyo sio ya kitaaluma ba hivo
hawatokuwa naye tena katika klabu hiyo
Anelka
kwa sasa yupo jijini Koweit katika shughuli za kidini aliachishwa
kazi mwezi Desemba mwaka 2013 katika klabu ya West Bromwich nchini
Uingereza kufuatia kuonyesha ishara ya ubaguzi dhifi ya wayahudi,
ishara ilioanzishwa na mchekeshaji wa Ufaransa mwenye utata Diedonne
na mbayo inayochukuliwa kuwa ni ya kibaguzi(Antisemite)
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire