Paul
Debbie, mshauri wa maswala ya Usalama kwenye Ofisi ya Umoja wa
Mataifa nchini Burundi ametajwa kuwa mtu asiye hitajika nchini
Burundi na kupewa muda wa saa 24 kuwa ameondoka nchini humo kuanzia
April 17 2014. Taarifa hii imetolewa kupitia mtandao wa kijamii wa
Twitter wa Ikulu ya Rais nchini Burundi.
Uamuzi
huu unatolewa baada ya siku mbili zilizopita Serikali ya Burundi
kuutaka Umoja wa mataifa nchini Burundi kuendesha uchunguzi wa kina
na kutowa mwanga kuhusu tuhuma ziliztolewa na umoja huo
zinazokituhumu chama tawala Tawala nchini humo kugawa silaha kwa
vijana wakereketwa wa chama cha CNDD-FDD maharufu Imbonerakure.
Akikutana
na mabalozi wenye makaazi yao nchini Burundi makam wa kwanza rais
Prosper Bazombanza aliutaka Umoja wa Mataifa kutowa ushahidi kuhusu
taarifa hiyo, la sivyo watachukuliwa hatuwa.
Wakati
huo huo Fetus Ntanyungu mbunge kutoka chama tawala ch CNDD-FDD
aliomba katika kikao cha Bunge kumtimuwa muakilishi wa katibu mkuu wa
Umoja wa Mataifa nchini Burundi Parfait Onanga Anyanga wakati Bunge
la taifa nchini humo lilipokuwa likijadili kuhusu Ofisi ya Umoja wa
Mataifa nchini Burundi BNUB.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire