Alexandre Niyungeko mkuu wa UBJ |
Polisi
nchini Burundi, imewazuia waandishi wa habari waliokuwa
wamepanga kufanya msafara wa amani wakati huu wakiandaa wiki mahususi
kwa ajili ya sherehe za siku ya wanahabari ambayo huadhimishwa Mei 3
ya kila mwaka.
Lengo la maandamano hayo ilikuwa ni kukemea kwa kauli moja uvunjifu wa sheria za uandishi wa habari na uhuru wa wanahabari nchini humo
Kulingana
na wanahabari nchini humo, msafara huo wa amani ulikuwa umepewa
idhini na pande zote husika, hususan wizra ya mambo ya ndani ilikuwa
imetowa taarifa kwa manispaa ya jiji lakini pia shirika la wanahabari
pia UBJ lilimuandikia risala Mea wa jiji ambaye aliridhia msafara huo
lakini wameseam hawaelewi kwanini msafara huo umesitishwa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire