Viongozi
wa serikali wa serikali ya Rwanda, wamesitisha mualiko wa Balozi wa
Ufaransa jijini Kigali Michel Flesch wa kuhudhuria kwenye maadhimisho
uya kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ya
mwaka 1994 na kumzuia kuiwakilisha Ufaransa.
Balozi
Flesch hatochukuwa tena nafasi ya waziri wa sheria Christiane Taubira
ambaye angeliongoza ujumbe wa serikali ya Ufaransa kwenye maadhimisho
hayo jijini Kigali.
Safari
ya waziri wa sheria wa Ufaransa na ujumbe wake kwenye maadhimisho
hayo ilisitishwa baada ya kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame
kuituhumu Ufaransa kuhusika moja kwa moja katika kupanga mauaji
mauaji hayo na kushiriki katika utekelezwaji wake.
Balozi
Flesch amesema hapo jana saa nne na nusu za usiku alipokea simu ya
waziri wa Rwanda anayehusika na mambo ya nje Louise Mushikiwabo
kwamba wamefuta mualiko wake, na hivo hapashwi kuhudhuria sherhe hizo
kwenye Uwanja wampira wa Miguu wa Amahoro jijini Kigali ambako Rais
Paul Kagame atazinduwa rasmi sherehe hizo.
Mbali
na kukataliwa kuhudhiria katika sherehe hizo, balozi Flesch amesema
amezuiliwa pia kwenda katika eneo la Ukumbusho Memorial huko Gisozi
kwa ajili ya kuweka shahada ya maua.
Ufaransa
ambayo ilikuwa mshirika wa karibu wa rais Habyarimana mwaka 1994 na
ambayo inatuhumiwa kuhusika katika mauaji hayo, imefuta ushiriki wake
katika sherehe hizo baada ya matamshi ya rais Paul Kagame na baadae
kufahamisha kwamba itawakilishwa na balozi wake jijini Kigali.
Mvutano
huu mpya baina ya serikali ya Kigali na Paris unaashiria kusitishwa
kwa harakati za kurejesha katika hali ya kawaida mauhusiano kati ya
mataifa haya mawili licha maridhiano yaliofikiwa mwaka 2010 na ambapo
mahusino yamekuwa sio imara. Katika mwaka 2010 Ufaransa ilikiri
kufanya makosa , lakini imekataa kuomba radhi kama inavyo ombwa na
Kigali.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire