Edouardo Dos Santos, eais wa Angola |
Rais wa
Angola Jose Eduardo Dos Santos anafanya ziara ya siku mbili hii leo
nchini Ufaransa, ikiwa ni ziara ya kwanza kutekelezwa na kiongozi
huyo kwa kipndi cha miaka kumi ikiwa na lengo la kuanzia ukurusa mpya
na kati ya paris la Luanda baada ya kuripotiwa kashfa ya uuzaji wa
Silaha kupitia kampuni ya angolaGate.
Dos
Santos ambaye husafiri mara chache sana ugenini, ambapo ziara yake ya
mwisho barani Ulaya ilikuwa nchini Ureno na Ujerumani mwaka 2009,
amekutana na rais wa Ufaransa Francois Hollande na kujadili kile
kilichotajwa na ofisi ya Ikulu ya rais jijini Luanda kufungua ukurasa
mpya na Ufaransa.
Uhusiano
kati ya Paris na luanda ulitiwa dowa mwaka 2000 baada ya kuwepo kwa
taarifa za uuzaji wa silaha kutoka kampuni ya Angolage wakati wa vita
vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 1975 hadi mwaka 2002.
Mahakama
ya Ufaransa ilifikia kikomo cha kashfa hiyo mwaka 2011. Mbali na
madhara hayo ya kidiplomasia, kashfa hiyo ilisababisha kukatishwa kwa
mikataba ya ma kampuni kama vile shirika la ndege la Air France,
kampuni ya mafuta ya Total.
Nchi
hizo mbili zimeanza kurejesha tena uhusiano wake mwaka 2008 ambapo
rais wa Ufaransa wa kipindi hicho Nicolas Sarkozy ambaye alionya kuwa
muda umewadia wa kufungua ukurasa mpya na kusahau yaliopita.
Octoba
iliopita waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius akiongoza
na ujumbe wa viongozi wa kampuni zaidi ya kumi na tano walizuru
jijini Luanda na kusisitiza umuhimu wa Paris kufunguwa ukurasa mpya.
Waziri
wa mambo ya nje wa Ufransa Laurent Fabius amemualika rais DAOS santos
pamoja na viongozi wa ma kampuni ya Ufaransa katika jukwa la
kibiashara ambalo limeandaliwa ikulu ya rais.
Ufaransa
ni mfadhili nambari tatu nchini Angola na ubadilishanaji wa kibishara
kati ya pande hizo mbili umefikia Euro milioni 680 katika mwaka 2012.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire