Ajouter une légende |
Jeshi
la Sudani Kusini limekiri kupoteza mji wa muhimu wa mafuta wa Bentui
uliorejea mikononi mwa waasi baada ya mapigano makali yalioshuhudiwa
tangu kipindi kadhaa.
Bentiu
mji mkuu wa jimbo la Unity, ni mji wa kwanza muhimu kutekwa na waasi
wanaomtii aliekuwa makam wa rais wa zamani nchini humo Riek Machar
baada ya mapigano makali yaliojiri mwishoni mwa mwaka uliopita ambapo
vikosi vya serikali vilifaanikiwa kuwafurusha waasi katika miji
muhimu.
Msemaji
wa jeshi la serikali ya Sudani Kusini Philip Agueir amesema waasi
wanaomtii Riek Mashar waliingia katika mji huo wa Bentiu tangu jana
jioni baada ya majeshi ya serikali kuondoka na kuwatuhumu waasi
kutekeleza mauaji ya kikatili dhidi ya raia wa kawaida.
Riek Mashar makam wa rais wa zamani ambaye ndiye kiongozi wa waasi |
Waasi
hao walikuwa wameuteka mji huo mwezi Desemba mwaka jana kabla ya
kuupoteza na kurejea tena mikononi mwa vikosi vya serikali.
Msemaji
huyo wa serikali amewatuhumu waasi kutekeleza mauaji Hospitalini,
sokoni ma miskitini, taarifa ambazo imekuwa vigumu kuthibitisha.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire