Mahakama
ya Kimataifa ya ICC imesema kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta sasa itaanza tarehe 7 mwezi Oktoba mwaka huu.
Rais
Kenyatta anashtakiwa na Mahakama hiyo kuchochea na kufadhili
machafuko ya baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 yaliyosabisha zaidi
ya watu elfu moja kupoteza maisha.
Kesi
dhidi ya Kenyatta ilistahili kuanza mwaka uliopita lakini kiongozi wa
Mashtaka Fatou Bensuda aliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo baada
ya kuituhumu serikali ya Kenya kukataa kushirikiana na Ofisi yake
kutoa taarifa za fedha za rais Kenyatta.
Majaji
wa ICC wameitaka serikali ya Kenya kuwasilisha taarufa hizo kwa Ofisi
ya Mwendesha Mashtaka ili kuendelea kwa kesi hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire