Mahakama
ya mjini New York nchini Marekani imemkuta na hatia shemeji wa
aliyekuwa kiongozi wa Kundi la Al-qaeda duniani Osama Bin Laden kwa
makosa ya kushirikiana na mtandao wa kigaidi kudhuru maisha ya
wamarekani.
Suleiman
Abu Ghaith, amekutwa na hatia ya kushiriki njama za kuua raia wa
Marekani na kuunga mkono ugaidi wakati akiwa kama msemaji wa kundi
hilo kati ya mwaka 2001 na 2002.
Abu
Ghaith sasa anakabiliwa na hukumu ya kifungo cha maisha kwenyeb
gereza la Marekani katika kesi iliyodumu kwa majuma matatu, kesi
ambayo ni ya kwanza ya juu kusikilizwa na mahakama ya kiraia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire