Rais wa Chile Michelle Bachelet |
Rais
mpya wa Chile, Michelle Bachelet ameapishwa hapo jana kwenye sherehe
zilizohudhuriwa karibu na viongozi wote wa kanda ya amerika kusini na
kaskazini huku akiahidi kuimarisha diplomasia kwenye taifa lake.
Akiwahutubia
wananchi, rais Bachelet ameonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa
kwamgawanyiko kati ya watu walionacho na wasio nacho, na kuongeza
kuwa suala lake la kwanza ambalo atalishughulikia ni kuleta usawa na
Umoja.
Kiongozi
huyo alirejea nchini mwake mwaka uliopita baada ya miaka minne kuwa
anatumika kwenye ofisi za Umoja wa mataifa UN.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire