Tume
maalumu iliyokuwa imeundwa kuchunguza kashfa ya rushwa na matumizi
mabaya ya fedha za walipa Kodi nchini Afrika Kusini, hatimaye hii leo
imetoa ripoti yake ya kumtaja dhahiri rais Jackob Zuma na mawaziri
wake kuhusika na ubadhilifi wa kiasi cha dola za Marekani milioni 23
za walipakodi.
Kiongozi
wa tume hiyo, Thuli Madonsela amesema kuwa tume yake imebaini kuwepo
mapungufu makubwa ya kisheria kwenye kuidhinisha matumizi ya fedha
zilizotumika kufanya ukarabati kwenye makazi ya rais Zuma na kutaka
awajibishwe kutokana na kushindwa kusimamia vema fedha za umma.
Thuli Madonsela |
Ripoti
hii inatolewa wakati huu ambapo rais Zuma anaendelea na kampeni zake
za kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi may mwaka huu, hatua
inayoelezwa kuwa ni pigo kwa utawala wake.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire