Viongozi
wa mataifa ya magharibi wameonyesha kwa mara nyingine tena uungwaji wao mkono kwa serikali mpya ya Ukraine na kupinga hatuwa ya
Urusi kurejesha eneo la Crimea kwenye himaya yake, ikiwa ni katika siku ya pili na ya mwisho ya mkutano wa unaofanyika jijini Hague
kuhusu Usalama.
Hapo
jana rais Barack Obama wa Marekani na washirika wake walifuta mkutano
wa G8 ambao ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Juni jijini Sotchi
nchini Urusi kama kupinga hatuwa iliochukuliwa na Urusi dhidi ya
Crimea ambapo tayari serikali ya Kiev imewaondowa wanajeshi wake
katika eneo hilo.
nchi
saba zenye utajiri mkubwa duniani G7 zimeitahadharisha Urusi kuhusu
hatuwa yoyote ambayo inaweza kuvuruga Usalama wa Ukraine.
Waziri
mkuu wa Uingereza David Cameron amesema wametuma ujumbe mzito wa
serikali ya Urusi, na kwamba vikwazo zaidi vitaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha Urusi inabadili msimamo wake.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire