Vikosi
vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na vikosi vya
Serikali ya Somalia wamefanikiwa kuikamata miji muhimu ya kusini mwa
nchi hiyo iliyokuwa inakaliwa na wanamgambo wa Al-Shabab wenye
uhisiano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Miji
ambayo imetwaaliwa toka kwenye mikono ya Al-Shabab ni ile iliyoko
kwenye mpaka wa nchi hiyo na Ethiopia, ambayo ni mji wa Wajid na
Hudur ambako waasi wa Al-Shabab walikuwa wamepiga kambi.
Wanajeshi
wa AMISOM wamesema kuwa, wameanzisha operesheni maalumu toka juma
lililopita kuwasaka wanamgambo hao kwenye miji ya kusini mwa nchi
hiyo, operesheni inayotekelezwa ikiwa zimepita siku kadhaa toka
wapiganaji wa Al-Shabab wafanye mashambulizi ya kujitoa muhanga mjini
Mogadishu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire