Hatua
ya Serikali ya Uganda kutia saini sheria mpya inayokataza mapenzi ya
watu wa jinsia moja nchini humo, imeelezwa na umoja wa Matiafa kuwa
huenda ikachangia kurejesha nyuma juhudi za taifa hilo kukabiliana na
maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Balozi
maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya
kupambana na maambukizi ya UKIMWI barani Afrika, Speciosa
Wandira-Kazimbwe ambaye pia aliwahi kuwa makamu wa rais wa Uganda,
amesema sheria hiyo inaongeza uwepo wa vitendo vya ubaguzi dhidi ya
jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Kazimbwe
amesema hatua hiyo inarudisha nyuma juhudi za Uganda kupambana na
maambukizi mapya, ambapo mwaka 2012 kulikuwa na wagonjwa milioni 1.5
pekee lakini kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wapya laki 1 na elfu
40.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire