Serikali
ya Uganda imeendelea kuwa kwenye shinikizo toka kwa mataifa ya
magharibi kufuatia hatua ya bunge na kisha rais Yoweri Museveni kutia
saini muswada wa sheria unaokataza ndoa za watu wa jinsia moja nchini
humo.
Safari
hii, bunge la Umoja wa Ulaya EU, limekubaliana kwa kauli moja
kuwawekea vikwazo vya kusafiri baadhi ya viongozi wa Serikali ya
Uganda ambao walihusika moja kwa moja na kupitisha sheria hiyo ambayo
wameikosoa.
Bunge
hilo sasa linapitia mapendekezo ya vikwazo ambavyo vinapaswa kuwekewa
rais wa Uganda Yoweri Museveni, spika wa bunge la Uganda, Rebecca
Kadaga na rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ambao wametejwa kwenye
muswada huo kuwa wamehusika moja kwa moja na kupitisha sheria hiyo
kandamizi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire