Serikali
ya Tanzania imetangaza kuwa hivi karibuni itatuma wanajeshi wake
kwenda nchini Sudan Kusini kulinda amani kufuatia ombi la katibu mkuu
wa Umoja wa Mataifa UN.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam Hapo jana, waziri wa mambo ya
kigeni wa Tanzania, Benard Membe, amesema nchi yake imekubali ombi la
Katibu mkuu Ban Ki Moon aliyeomba nchi hiyo itume wanajeshi wake
nchini Sudan Kusini kusaidia kulinda amani.
Waziri
Membe amesema kuwa kutokana na mchango wa vikosi vya Tanzania nchini
Jamhuri ya Kidekrasia ya kongo, Umoja wa Mataifa umeona uiombe tena
nchi ya Tanzania kutuma wanajeshi wake Sudan Kusini.
Hata
hivyo waziri Membe hakusema ni lini hasa wanajeshi hao wataondoka
Tanzania kuelekea Sudan Kusini.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire