Umoja
wa mataifa UN umeonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa ongezeko la
mashambulizi ya kushtukiza yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la
Al-Shabab nchini Somalia wakati huu ambapo operesheni kubwa inafanywa
kukabiliana na wapiganaji hao.
Balozi
maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Somalia, Nicholas Kay amesema
kuwa licha ya operesheni kubwa inayoendelea kufanywa na vikosi vya
Umoja wa Afrika AMISOM kuwadhibiti wapiganaji hao, bado wanamgambo wa
Al-Shabab wameendelea kuwa na nguvu na kuzidisha mashambulizi yao
mjini Mogadishu.
Kay
amesema kuwa wanamgambo hao wameshajua kuwa wamezidiwa kwenye vita
hivyo na ndio maana na wao wameendelea kuzidisha mashambulizi zaidi
dhidi ya vikosi vya Serikali na wanajeshi wa AMISOM.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire