Waasi
wa jeshi huru nchini Syria wameanzisha mapigano makali dhidi ya
wanajeshi wa Serikali ya rais Bashar al-Asad kwenye miji minne
mikubwa ambayo awali waliipoteza kwenye mikono ya serikali.
Operesheni
hii ya waasi wa Syria inaelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni hatua
ya ulipizaji kisasi dhidi ya operesheni za Serikali ambazo
zilifanikisha kuwapokonya miji hiyo na sasa wanajaribu kuirejesha
kwenye himaya yao.
Katika
hatua nyingine katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon
amesema hali ya misaada ya kibinadamu nchini Syria hasa kwenye miji
yenye mapigano bado imeendelea kuwa changamoto kwakuwa bado
wafanyakazi wa mashirika ya misaada wanashindwa kufika kwenye maeneo
hayo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire