Rais
wa Urusi, Vladmir Putin ameendelea kutia ngumu dhidi ya vitisho na
vikwazo ilivyowekewa nchi yake na mataifa ya magharibi kufuatia hatua
yake ya kulitambua eneo la Crimea kama sehemu yake, akisema vitisho
hivyo vinachukuliwa kama vita kwa nchi yake.
Akiwahutubia wabunge wakati wa sherehe za utiaji saini makubalino rasmi ya kulitambua eneo hilo kama sehemu ya Ukraine, rais Putin amesema nchi yake hitatishwa na vikwazo vya mataifa ya magharibi na kusisitiza kuwa Crimea ni sehemu na itaendelea kuwa eneo la Urusi na kamwe hawatotenganishwa na yeyote.
Kauli ya Putini pamona na kutia saini mkataba na viongozi wa Crimea waliokuwepo wakati wa hotuba hiyo, inaonekana kama ubabe wa nchi yake kutaka kuyaonyesha mataifa ya magharibi kuwa inalenga kulikamata eneo hilo na haina nia ya kusalimisha nia yake kwa viongozi hao.
Hatua hii ya Urusi inaelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa itaendelea kuamsha hasiara zaidi ya viongozi wa mataifa ya magharibi na huenda kukawa na athari kubwa kwa Urusi na dunia.
Picha kwa Hisani ya Chinanews.com
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire