Kiongozi
mmoja wa chama cha upinzani cha Uprona nchini Burundi ameponea
chupuchupu katika shambulio la guruneti lililotokea katika usiku wa
jana kuamkia leo jumatatu, tukio ambalo linadaiwa kuwa ni ulipizaji
kisase dhidi ya mzozo ulipo katika chama hicho. Chama Uprona
kilijigawa makundi 2, Upande wenye wafuasi wengi kilijiondowa katika
serikali kikipinga hatuwa ya serikali kuingilia kati katika taasisi
zake za uongozi, huku upande mwingine ukionekana kuwa karibu zaidi na
chama tawala cha CNDD-FDD.
Gaston
Sindimwo mmoja kati ya viongozi wa chama Uprona kinachounga mkono
serikali amesema alishambuliwa na guruneti wakati alipojaribu kutoka ndani mwake kwa lengo la kuchukuwa begi alilokuwa amecha ndani ya
gari lake, ndipo vijana wawili ambao amesema walionekana kumlenga na
kumrushia guruneti ya kwanza iliofuatiwa na nyingine ya pili.
Hata
hivyo vigaye vya guruneti hizo ndivyo vilivyo mjeruhi mgomgoni na
sasa anaendelea vizuri. Ameelekeza kidole cha lawama kwa upande
mwigine wa chama hicho na kusema kwamba wao ndio wanaohusika na tukio
hilo la kutaka kumuondowa duniani.
Upande
huo wa chama Uprona uliojindowa serikalini umetupilia mbali tuhuma
hizo. Kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho Tatien Sibomana, kuuwa sio
mingoni mwa sera za chama Uprona kwa kuwa hakuna faida yoyote kwani
Chama cha CNDD-FDD kinaweza kumbadili mara moja. Tatien Sibomana
ameitaka polisi nchini humo kutotumia fursa hii na kuanza kuwakamata
watu kiholela kwa kuwashukia kuhusika na tukio hilo.
Mzozo
ulioibuka katika chama Uprona moja kati ya vyama vyenye wafuasi wengi
wa kitutsi na chama tawala cha CNDD-FDD chama cha uasi zamani chenye
wafuasi wengi wa kabila la watutsi, unatishia shughuli za ugavi wa
madaraka kati ya watutsi waliowachache na wahutu waliowengi ambapo
mchakato wa maridhiano unasuasua tangu miongo kadhaa.
Wachambuzi
wa maswala ya siasa wanaokuwa mzozo huu wa pande hizi mbili ni ishara
tosha kwamba rais Nkurunziza yupo tayari kwa hali na mali kuwania
muhula mwingine watatu katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire