Hofu
ya kushuhudiwa mgawanyiko zaidi ndani ya chama kikuu cha upinzani
nchini Zimbabwe cha Movement for democratic Change MDC, imeendelea
kutanda wakati huu ambapo uongozi wa chama hicho ukiwataka viongozi
waliochoka kuwemo ndani ya chama hicho kujiondoa wenyewe.
Msimamo
wa chama hicho umetolewa mwishoni mwa juma na rais wake, Morgan
Tsvangirai ambaye ameendelea kusisitiza kuwa hatoondoka madarakni kwa
shinikizo la viongozi wachache wenye kutaka kumpindua.
Kauli
ya Tsvangirai ameitoa ikiwa zimepita siku mbili tu, toka chama hicho
kitangaze kumsimamisha kwa muda naibu mweka hazina wa chama hicho,
Elton Mangoma kufuatia matamshi yake ya hivi karibu kumtaka kiongozi
huyo kujiuzulu.
Mangoma
sasa anasubiri uamuzi wa kamati ya nidhamu ya chama hicho ambayo
itaketi hivi karibuni kuamua hatma yake.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire