Mamilioni
ya watu walionaswa kwenye mapigano nchini Sudan Kusini wanakabiliwa
na hali mbaya ya chakula wakati huu msimu wa mvua ukikaribia, hii ni
kwa mujibu wa ripoti moja ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya
kibinadamu nchini humo.
Mkuu
wa tume ya kuratibu misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, John
Ging amesema nchi hiyo inakabiliwa na baa la njaa kutokana na uhaba
wa chakula hali inayowafanya wananchi wengi zaidi kuwa kwenye hatari
ya kupoteza maisha.
John
Ging amesema licha ya kuwa hawajatangaza hali ya njaa nchini Sudan
Kusini lakini ukweli wa mambo unaonesha dhahiri taifa hilo kuelekea
huko na pengine kushuhudia hali hiyo ikitangazwa.
Kiongozi
huyo ametaka kusitishwa kwa mapigano ili kutoa nafasi ya wananchi
kupokea misaada ya kibinadamu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire