Mamlaka
nchini Libya zimesema kuwa wamefanikiwa kuizua meli ya mafuta ya
Korea Kaskazini iliyokuwa ikijazwa mafuta kwenye bandari ya
Al-Sidra, bandari ambayo inamilikiwa na kundi moja la waasi.
Hapo
jana utawala wa Tripoli ulitangaza kuwa ungeingilia kati zoezi ambalo
lilikuwa linatekelezwa na waasi hao kwa kile serikali inachodai kuwa
waasi hao hawana haki ya kuuza mafuta na yeyote atakayefanya kinyume
na hapo atakumbana na vikwazo.
Waziri
mkuu wa Libya Ali Zeidan amethibitisha wanajeshi wa Serikali
kuidhibiti Meli hiyo, na kwamba leo asubuhi wameanza kuisindikiza
kuelekea bandari ya mashariki ambayo inamilikiwa na serikali na
kwamba watu waote waliokuwemo kwenye meli hiyo watachukuliwa hatua za
kisheria.
Hata
hivyo waasi hao wamekanusha meli hiyo kuzuiwa na vikosi vya Serikali.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire