Polisi nchini Burundi iliendesha shambulizi mwishoni mwa juma lililopita katika makazi ya chama cha upinzani chga MSD kwa lengo la kuwakamata wafuasi wa chama hicho pamoja na mwenyekiti wake Alexis Sinduhije waliokuwa wamewateka polisi wawili.
Watu
zaidi ya ishirini walijeruhiwa katika tukio hilo wakiwemo vijana wa
chama hicho cha MSD pamoja na polisi watatu.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka nchini Burundi, tukio hilo lilianza mapema
asubuhi siku ya Jumamosi wakati vijana wa chama hicho waliokuwa
wamevalia vitamba vya chama walipoluwa wakifanya mazoezi wakielekea
mjini kati. Ghafla wakakumbana na polisi ambo waliwasambaratisha, na
kuwakamata miongoni mwao ambao walipelekwa moja kwa moja katika jela
kuu la Mpimba, huku wengine wakitimkia katika ofisi za chama cha MSD
kusini mwa jiji kuu Bujumbura huku polisi ikuwafuata kwa kutumia bomu
za kutowa machozi nao wakijibu kwa kurusha mawe.
Katika
vurugu hizo polisi wawili walitekwa na vijana hao na kufungwa katika
moja ya vyumba vya ofisi. Mwenyekiti wa chama cha MSD Alexis
Sinduhije alitetea hatuwa hiyo na kudai kuwa vijana wamejihami baada
ya polisi kuwashambulia kwa lengo la kuwauawa, na kuongeza kuwa
kamata kamata ya watu kiholela lazima isitishwe, huku akikumbusha
kuwa rais Nkurunziza hayupo juu sheria, na kwamba hawatokubali tena,
watasimama hadi mwisho na ataendelea kusimama kidete akiwa huru au
amekufa.
Shambulio
baada
ya kuwateka nyara polisi hao, hali ilibadilika na kuanza kuwa mbaya.
Alexis Sinduhije alilazimisha kuachiwa huru kwa wafungewa wa kisiasa
kama vile El haj Hussein Rajabu , Frederic Bamvuginyuvira pamoja na
wale wote ambao tayari wamemaliza robo ya kifungo kabla ya kuwaacha
huru polisi hao.
Wakati
huo polisi walikuwa wamekusanyika mbali kidogo na eneo hilo wakiwa na
silaha. Ndani ya ofisi za chama, vijana wafuasi wa chama walikuwa
wanaimba nyimbo za kukitukuza chama chao.
Saa
kumi jioni, wanaharakati wa mashirika ya kiraia hususan mkuu wa chama
kinacho tete haki za wafungwa APRODH Pierre Claver Mponimba alijaribu
kuendesha usuluhishi kati ya Alexis Sinduhije na ma afisa wa Polisi
bila mafaanikio. Alimtaka Sinduhije kuwaacha huru polisi hao ili
kuepusha mashambulizi. Saa moja baadae wafuasi wa chama hicho
walikubali kukabidhi silaha mbili walizokuwa nazo kutoka kwa polisi
hao waliowashikilia mateka aina ya AK40 na kusalia na radio zao za
mawasiliano.
Saa
kumi na moja na nusu, polisi iliamuwa kuendesha shambulio kwa kutumia
bomu za kawaida pamoja na za kutowa machozi, huku milio ya risase
ikisikika kwa wingi na kudai kuwa vijana wa chama cha MSD ndio
waliaonza kurusha risase. Baada ya muda wa zaa nzima za makabiliano,
polisi walifaulu kuiteka ofisi hiyo, huku mwenyekiti wa chama Alexis
Sinduhije na wafuasi wake wa karibu wakafaanikiwa kutoroka. Vijana
kadhaa wa chama cha MSD walitiwa nguvuni, mateka hao polisi
waliachiwa huku ofisi za chama hicho zikilindwa na polisi.
Picha kwa Idhni ya Gazeti la Iwacu
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire