Walinzi
wa tatu wa karibu sana wa rais Barack Obama wa Marekani ziarani
barani Ulaya, warejeshwa nyumbani baada ya kukutwa wamelewa kupita
maelezo. Afisa hao wa ulinzi kutoka idara ya ujasusi walirudishwa
jijini Washington Jumapili iliopita siku moja kabla ya kuwasili wa
rais Obama jijini Amsterdam. Gazeti la Washington Post lililovumbua
taarifa limesema mmoja kati ya maafisa hao alikutwa amelewa chepe
huku hajitambuwi baranai karibu na Hoteli walikokuwa wamefikia.
Maafisa
hao wote wa tatu ni kutoka kitengo maalum cha idara ya Ujasusi
kinacho husikana ulinzi wa Rais wa Marekani iwapo itatokea
shambulizi. Kazi yao wanahusika na kubaki kwenye eneo la tuko na
kujibu mashambulizi, wakati kundi nyingine likihusika na kumlinda
rais kwa kumuondowa haraka sana kwenye eneo la tukio. Kundi hilo la
maafisa wanaojibu mashambulizi, ni la maafisa walioajiriwa kutokana
na kuwa na uwezo wa na ujuzi wa hali ya juu.
Wanajeshi
hao wanatuhumiwa kuvunja sheria inayo tumiwa kwa maafisa wote wa
ulinzi wa rais Barack Obama: kutojihusisha na kilevi chochote kwa
muda wa saa kumi kabla ya kuanza shughuli.
Maafisa
hao walifanya sherehe kwa pamoja siku ya Jumamosi, wakiwa na dhamira
ya kurejea katika hali ya kawaida kabla ya kutuwa kwa ndege ya Air
Force One, Jumatatu March 24 asubuhu, hawakupima muda wa kilevi
walichotumia na hivo kutokea kwa hali hiyo iliosababisha mmoja kati
ya walinzi kuwasiliana na ubalozi wa Marekani.
Gazeti
la Washington Post, limekumbusha kuwa, Sheria ihusuyo kanuni ya
maafisa wa ujasusi ilibadilishwa mwaka 2012 baada ya kutokea kwa
kashfa nchini Colombia ambapo maafisa 10 waliachishwa kazi baada ya
kuwasiliana na kituo kimoja cha Makahaba. Hasira ya chini kwa chini
ya rais Barack Obama ndio ilioplekea kujiuzulu kwa mkurugenzi wa
Idara ya ujasusi wa Marekani
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire