Wanaharakati
na wanasiasa wanaotetea ndoa za watu wa jinsia moja, hapo jana
wamewasilisha rasmi kesi mahakamani kupinga sheria iliyotiwa saini na
rais Yoweri Museveni kukataza mapenzi ya watu wa jinsia moja.
Mmoja
wa wabunge walioshiriki kuwasilisha kesi hiyo kwenye mahakama kuu,
amesema kuwa wao wanaamini kuwa sheria hiyo ni kandamizi na inalenga
kuminya uhuru wa demokrasia nchini humo ikiwemo wa watu kupendana na
kufanya vitu vyao kwa uhuru bila kubugudhi wengine.
Wanaharakati
wa kutetea haki za binadamu nchini Uganda wanapingasheria hiyo
wanayodai inakikuka haki za binadamu, sheria ambayo hata mataifa ya
magharibi yanayotoa msaada wa kwa nchi yametangaza kusitisha baadhi
ya misaad.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire