Takribani
watu wanne wameuawa katika mapigano ya Jumamosi mjini Bangui wakati
ambapo vikosi vya jeshi la Kifaransa vilipoingilia makabiliano kati
ya makundi ya wapiganaji.
Afisa
wa jeshi la Umoja wa Afrika ambaye hakupenda jina lake litajwe a amesema kuwa Watu wanne,
ikiwa ni pamoja na waislamu 2 waliuawa huku wengine saba wakijeruhiwa
katika mapigano kati ya vikundi vyenye silaha, ikiwa ni pamoja na
kundi la anti Balaka.
Afisa
huyo aliongeza kuwa Mapigano yalizuka katika maeneo kadhaa kwa wakati
mmoja na kusababisha jeshi la kimataifa kuingilia ili kukomesha
mauaji lakini nayo yakawa sehemu ya mapigano.
Chanzo
kimoja kutoka Jeshi la kifaransa kimearifu kuwa mapigano kati ya
vikundi vyenye silaha dhidi ya jeshi hilo yameripotiwa ambapo
wanajeshi hao wamejipanga kukabiliana nao kwa vile walishambuliwa na
kujibu mashambulizi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire