Watu
wanne wamepoteza maisha na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa katika
shambulio lilitokea jana ndani ya kanisa moja jijini Mombasa baada ya
watu wenye silaha kuingia kanisani na kuanza kuwavurumishia risase
waumini.
Shambulio
hilo linakuja wakati huu polisi katika eneo hilo ikijinasibu
kuimarisha Usalama na kuwa tayari kujihami dhidi ya mashambulizi ya
wanamgambo wa Al Shabab.
Kiongozi
wa polisi katika Wilaya ya Likoni kusini mwa jiji la Mombasa Robert
Mureithi amesema watu wawili walipoteza maisha papo hapo huku
wengine wawili wakiuawa baada ya kufikishwa Hospitalini.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire