Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa |
Baraza
la usalama la Umoja wa Mataifa UN limeonya kuhusu kuendelea kuzorota
kwa hali ya usalama mjini Mogadishu nchini Somalia kufuatia
mashambulizi yanayotekelezwa na wapiganaji wa Al-Shabab.
Hapo
jana balozi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Somalia, Nicholas
Kay alilazimika kukatisha safari yake
kuelekea mjini Mogadishu kufuatia kuonywa kuhusu usalama kwenye nchi
hiyo.
Akiwahutubia
wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa njia ya video
akiwa mjini Nairobi, Kenya, balozi Kay amewaambia wajumbe kuwa hali
ya usalama nchini Somalia si yakuridhisha tena licha ya sehemu kubwa
ya wanamgambo wa Al-Shabab kudhibitiwa.
Balozi
Kay anataka hatua zaidi kuchukuliwa na Umoja wa mataifa kudhibiti
hali ya usalama nchini humo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire