Kesi
ya maafisa wakuu wanne wa chama cha SPLM wanaotuhumiwa ugaidi, uasi
na jaribio la kuipindua serikali ya Rais Salva Kiir imeanza
kusikilizwa jana mjini Juba nchini Sudani Kusini.
Watuhumiwa
hao ni Pagan Amum, katibu mkuu wa zamani wa SPLM, Waziri wa zamani wa
Usalama Oyai Deng Ajak, Ezekiel Lol Gatkuoth aliyekuwa Balozi wa
Sudan Kusini nchini Marekani na Naibu waziri wa ulinzi Makaj D' Agoot
ambao ni washirika wa karibu wa Riek Machar , aliyekuwa makamu wa
rais.
Mawakili
wa watuhumiwa hao wanazungumzia kesi hiyo kuwa ya kisiasa na njama za
kuwadhoofisha wanasiasa hao nchini humo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire