Pages

vendredi 21 mars 2014

MAKAM WA RAIS WA ZAMANI NCHINI BURUNDI FREDERIC BAMVUGINYUNVIRA AACHIWA HURU KWA DHAMANA KUTOKANA NA SABABU ZA KIAFYA



Frederic Bamvuginyumvira

Mahakama kuu inayo pambana na rushwa nchini Burundi, imemuachia huru kwa dhamana aliyekuwa makam wa rais wa zamani nchini humo Frederic Bamvuginyuvira kutokana na sababu za kiafya. Bamvuginyumvira alikamatwa Desemba 5 mwaka 2013 kutokana na kuhusishwa katika tukio la kutembea nje ya ndoa yake na baadae kujaribu kutowa rushwa.

Wakili wa Frederic Bamvuginyunvira Fabien Segatwa amesema mahakama inahusika na kupambana na rushwa imemuachia huru kwa dhamana mteja wake baada ya kutowa dhamana inayo lingana na franka za Burundi milioni moja, sawa na Euro 450.

Wakili Fabien Segatwa

Duru kutoka katika mahakama hiyo zimearifu kwamba Banvuginyumvira ameachiwa huru kwa dhamana kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu (Presha)

Wakili Segatwa amesema wameridhishwa na hatuwa hiyo kwani mteja wake hana sababu zozore za kusalia korokoroni kwakuw ahana hatia yoyote, anazuiliwa kutokana na sababu za kisiasa, hii itamsaidia kujitibisha na kujitetea kikamilifu. 

Frederic Bamvuginyumvira mwenye umri wa miaka 52 alikamatwa katika nyumba moja ya wageni akiwa na mwanamke mwenye umri wake, na baadae kutuhumiwa kosa la rushwa, kwa kumshawishi afisa polisi aliyemkamata ili amuachiye huru.

Katika tukio hilo, upinzani nchini Burundi inaituhumu serikali kubuni mbinu za kumuangusha kisiasa mwanasiasa huyo ambaye anaonekana huenda akawa tishio katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Kwa sasa Frederic Bamvuginyuvira ambaye ni naibu mwenyekiti wa chama cha FRODEBU anazaniwa kuwa ndiye mgombea mmoja wa upinzani katika uchaguzi wa mwaka 2015. Anchukuliwa kama mtu mwenye upinzani mkubwa sana kwa rais Pierre Nkurunziza ambaye anaonyesha nia ya kuwania muhula mwengine wa tatu.



Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...