Mamlaka
nchini Msumbiji imewataka wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya kusini
mwa nchi hiyo hasa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko, kuhama nyumba zao
kuhofia madhara zaidi yanayoweza kutokea.
Tangazo
la Serikali linatolewa wakati huu ambapo wananchi wa miji ya
Fevereiro ambao wanaishi jirani na mto, Icomati wakikabiliwa na hali
mbaya ya kibinaadamu kutokana na maeneo mengi kukumbwa na mafuriko.
Kitengo
cha maafa nchini Msumbiji kimesema kuwa zaidi ya watu elfu sita
wanaoishi jirani na eneo la mto Icomati wanakabiliwa na hali mbaya na
kwamba wasipohama hara kwenye maeneo yao huenda wakakumbwa na
mafuriko zaidi na kupoteza maisha.
Mpaka
sasa hakuna madhara ya watu kupoteza maisha yaliyoripotiwa na
serikali kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire