Kesi ya mauji inayomkabili mwanariadha mwenye ulemavu wa miguu raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, imeingia wiki ya pili ambapo upande wa mashtaka umeendelea kuwasilisha ushahidi zaidi kuonesha mwanariadha huyo kumuua mchumba wake kwa makusudi.
Hapo
jana mwendesha mashtaka alimwita kizimbani daktari aliyeufanyia
uchunguzi mwili wa Reeva Steenkamp ambapo alielezea majeraha
aliyokuwanayo mchumba wa Pistorius baada ya kushambuliwa kwa risasi
hali iliyomfanya hata Oscar Pistorius kushindwa kujizuia na kuanza
kutapika wakati ushahidi huo ukiwasilishwa.
Pistorius
anatuhumiwa kupanga njama za kumuua mchumba wake tarehe 14 ya mwezi
February usiku wa kuamkia siku ya wapendanao, ambapo jana pia
ushahidi mpya ulitolewa kuonesha kuwa wapenzi hao walikuwa wameamka
wote wakati wa tukio tofauti na maelezo ya Pistorius aliyoyatoa
awali.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire