Waziri
wa mambo ya ndani wa Burundi Edourd Nduwimana amefahamisha kwamba
wale wote wanaopinga rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu kwa
kufurahishwa kuona muswada wa marekebisho ya katiba umekwamishwa
bungeni, hili halitamkwamisha Nkurunziza kuwania uchaguzi wa rais wa
mwaka 2015 ujao. Hii ni mara ya kwanza waziri wa Mambo ya ndani
kutangaza rasmi kuwa rais Nkurunziza atawania uchaguzi mkuu, na hivo
kuzua mtafaruku kuhusu swala hili linalo wakera wengi.
Rais
Nkurunziza alikuwa amejizuia kwa kipindi chote hichi kutamka rasmi
kwamba atakuwa miongoni mwa wagomnbea kiti cha urais katika uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015.
hatuwa
ya hivi majuzi ya bunge la taifa hilo kutupilia mbali muswada wa
mapendekezo ya katiba ya nchi hiyo ili kumpa nafasi ya kuwania tena
muhula mwingine wa tatu, ndiyo ambayo imebadili kalenda, na hivo
waziri wa mambo ya ndani ambaye ni mtu wa karibu na utawala kupewa
nafasi ya kuweka wazi kwa mara ya kwanza kuhusu hatuwa hii ya rais
kuwania uchaguzi wa mwaka 2015.
Waziri
nduwimana amesema “kile
tunachopinga ni kuona kwamba kuna watu wanaoona kuwa swala la rais
Nkurunziza kuwania uchaguzi mkuu kwa muhula wa tatu limekwisha, la
hasha sio kweli. Kile ninacho washauri wanasiasa wataowania uchaguzi
ni kujiandaa huku wakitambuwa kwamba watapambana na rais wa sasa.
Mahakama ya kikatiba ndiyo itayo amuwa kwa njia moja ama nyingine na
wananchi watatakiwa kuheshimu maamuzi.”
Waziri
wa mambo ya ndani wa Burundi ameanzisha mjadala huu kuhusu muhula wa
tatu wa rais Nkurunziza ikiwa ni takriban wiki moja baada muswada wa
mabadiliko ya katiba kukwama bungeni. Waziri wa mambo ya ndani yeye
anasema rais Nkurunziza anawania muhula wa pili kwakuwa katika
uchaguzi wa mwaka 2005 alichaghuliwa na bunge, na hivo muhula ulipo
sasa ndio muhula wa kwanza. Mahakama ya kikatiba ndiyo itayo amuwa
kuhusu hatuwa hii.
Hii
inakuja baada ya kushindwa kwa hatuwa ya kwanza, utawala wa Burundi
umeanzisha mvutano dhidi ya upinzani unaopinga katu katu kusikia kuwa
Nkurunziza anajichaghulisha tena katika muhula wa tatu, na ambao
wanasema hawana imani na mahakama ya kikatiba ambayo tayari imesha
onyesha upendeleo na unaundwa na watu kutoka chama tawala.
Pour
le parti de l’opposition, l’Union pour le progrès national
(Uprona), ce recours à la Cour constitutionnelle est une nouvelle
tentative de « passage en force » de la part du
président. Selon l’article 96 de la Constitution de mars 2005,
basée sur les accords d’Arusha ayant permis de mettre fin à la
guerre civile burundaise (1993-2006), le président « est élu au
suffrage universel direct pour un mandat de cinq ans renouvelable une
fois ».
Joint
par RFI, Charles Nditijé, le président de l'Uprona estime qu'il
faudra s'opposer à cette « violation de la Constitution »
: « C’est
vraiment la voie de la confrontation qu’il ont décidé d’emprunter
depuis le processus d’amendement de la Constitution. Les
représentants du peuple viennent de refuser ces amendements qui
offrent sur un plateau d’argent un troisième mandat au président
de la République. Aujourd’hui, la Constitution est claire ;
l’accord d’Arusha est clair. Nous devons nous préparer à
refuser ce diktat, ce passage en force et cette imposition ».
Chama
cha Upinzani cha Uprona kinasema kukimbilia katika mahakama ya
kikatiba ni hatuwa nyingine ya pili ya matumizi ya nguvu yanayo
tumiwa na rais. Kwa mujibu wa kifungu nambari 96 cha katiba ya March
mwaka 2005 iliofikiwa chini ya makubaliano ya amani ya jijini Arusha
yaliopelekea kusitishwa vita vya wenywe kwa wenyewe vya mwaka
1993-2006, rais wa jamhuri anachaguliwa kupitia kura za wananchi kwa
kipindi cha miaka mitano ambayo inaweza kuongezwa mara moja.
Akizungumza
na RFI, Charles Nditije mwenyekiti wa chama Uprona amesema inafaa
kupinga kwa nguvu zote uvunjifu huu wa katiba ambao unaendelea
kutekelezwa na chama tawala, wakati ambapo katiba ipo wazi, mkataba
wa amani wa Arusha upo wazi, kwa hiyo amesema hatuwa hii ni ya
kutupilia mbali.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire