Upinzani
nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC unapinga mchakato
unaodaiwa kuanza ndani ya chama tawala nchini humo cha PPRD ambapo
viongozi wake wanalenga kukusanya saini zaidi ya laki 1 ili kumpa
nafasi rais Joseph Kabila kuendelea kusalia madarakani hata baada ya
mwaka 2016.
Hapo
jana katibu mkuu wa chama cha PPRD, Claude Mashala amewaambia
wanahabari kuwa wameanzisha harakati za kukusanya saini hizo ili
kubadili katiba ya nchi hatua ambayo imepingwa vikali na upinzani
ambao unasisitiza rais Kabila kutowania tena urais.
Hata
hivyo spika wa bunge la DRC Aubin Minaku amenukuliwa hii leo
akisisitiza kuwa rais Josephu Kabila hana mpango wa kuongeza muda wa
yeye kusalia madarakani baada ya muda wake kukamilika.
Wachambuzi wa masuala ya siasa akiwa mjini Goma mashariki
mwa DRC na hapa anasema mara nyingi rais anaweza asiwe yeye ameamua
bali ni ushawishi wa baadhi ya watu jambo ambalo ni hatari.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire