Kushoto ni aliyekuwa waziri mkuu Ali Zeidan na Kulia ni aliyekuwa waziri wa Ulinzi Abdoullah Ali Thani |
Serikali
ya Libya imemziwia aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan kwa
kumtuhumu kuhusika katika vitendo vya kupitisha mlango wa nyuma mali
za serikali. Vyombo vya habari nchini Libya vimesema hatuwa hiyo
imechukuliwa huku waziri mkuu huyo was zamani akiwa tayari kaondoka
nchini
Hatuwa
hii imekuja baada ya wabunge 124 kati ya 194 wanaounda bunge la
nchini Libya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri huyo ambaye
nafasi yake imechukuliwa na waziri wa Ulinzi Abdoullah Al Thani
ambaye aliapishwa jana kuongoza serikali hadi pale atapo chaguliwa
waziri mkuu mwingine.
Hii
inakuja baada ya waziri huyo kushindwa kutatua mzozo wa Meli ya Korea
kaskazini ilioegesha katika eneo la Al Sindra linalo dhibitiwa na
waasi likiwa na takriban pipa 234.000 za mafuta.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire