Ikiwa
ni siku mbili zimepita toka waziri wa mambo ya ndani wa Burundi,
Edouard Nduwimana kutangaza kukifungia kwa miezi minne chama cha
upinzani cha MSD, kinachoongozwa na Alexis Sinduhije, mashirika ya
kutetea haki za binadamu pamoja na wanahabari nchini humo
wamemuandikia barua ya wazi rais wa jamhuri, Pierre Nkurunziza
kuzingatia suala la usalama wa nchi.
Tamko
hilo la mashirika ya kiraia yenye uhisiano na mahakama ya kimataifa
ya uhalifu wa kivita ya ICC pamoja na wanahabari, limekuja kufuatia
madai yao kuwa serikali inalenga kuminya uhuru wa demokrasia kwa
kuzuia vyama vya siasa kutekeleza majukumu yao pamoja na wanahabari
kuripoti habari zao hali inayotishia uwezekano wa kutokea vurugu
nchini humo hata kabla ya uchaguzi mkuu.
Wachambuzi
wa masuala ya siasa nao wanaona kuwa bado hali ya demokrasia nchini
Burundi ni tete na imewekwa rehani na watu wachache
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire