Waziri wa sheria nchini Afrika Kusini Jeff Radebe |
Serikali
ya Afrika Kusini imezungumzia kwa mara ya kwanza kuhusu mgogoro wa
kidiplomasia baina yake na nchi ya Rwanda.
Afrika
Kusini imeionya nchi ya Rwanda na kudai kuwa ardhi yake haitatumika
kama uwanja wa vita kati yake na mataifa ya magharibi siku chache
baada ya taifa hilo kuwafurusha maofisa wake watatu wanaotuhumiwa
kupanga njama kuwashambulia wanasiasa wa Rwanda wanaoishi nchini
humo.
Akizungumza
na wanahabari mjini Pretoria, waziri wa sheria, Jeff Radebe amesema
kuwa kamwe nchi yake haitakubali kuona taifa lolote lile duniani
likitumia ardhi yake kufanya shughuli zozote ambazo zinahatarisha
usalama wa nchi na raia wake.
waziri
huyo amesema kuwa wana ushahidi kuwa maafisa wa ubalozi wa Rwanda na
mmoja wa Burundi wamehusika katika majaribio ya mauaji ikiwemo ya
mpizani mmoja kutoka Rwanda.
Hivi
karibuni makazi ya Jenerali Kayumba Nyamwasa yalishambuliwa na kabla
ya hapo mapema mwaka huu, aliyekuwa mkuu wa upelelezi nchini Rwanda
Patrick Karegeya alekutwa ameuwawa katika hoteli moja mjini
Johannesburg.
Louise Mushikiwabo waziri wa mambo ya nje nchini Rwanda |
Katika
hatua nyingine Serikali ya Rwanda imejibu mapigo kupitia waziri wake
wa mambo ya Kigeni, Louis Mushikiwabo ambaye kupitia mtandao wa
Twitter ameitaka Afrika kusini kuacha kuwapa hifadhi wahaini wa nchi
hiyo ama sivyo ikubali gharama ya kile kinachotokea.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire