Kiongozi
mpya wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis hii leo anatimiza mwaka
mmoja toka achaguliwa kushika nafasi hiyo, huku akijipatia umaarufu
duniani kutokana na mabadiliko makubwa anayoyafanya ndani ya kanisa
hilo.
Toka
ameingia madarakani, Papa Francis amekuwa ni tofauti na viongozi
wengine waliomtangulia, ambapo alikataa hata kuishi kwenye makazi
yake ya kifahari ya mjini Vatican na badala yake anaishi kwenye
nyumba moja ya kulala wageni jirani na makao makuu ya kanisa hilo.
Mbali
na kuishi kwenye nyumba ya kawaida kiongozi huyu pia amekuwa ni mtu
wa watu ambapo amekuwa akijichanganya na watu masikini, na wakati
mmoja alitajwa kama moja kati ya watu maarufu duniani na gazeti la
Forbes.
Wachambuzi
wa masuala ya Theolojia wanasema kuwa kiongozi huyu ataendelea kuwa
maarufu kutokana na kujaribu kufanya mabadiliko ya ndani ya kanisa
ikiwa ni pamoja na kukabiliana na kshfa dhidi ya makasisi wake
wanaotuhumiwa kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji watoto.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire