Katibu mkuu wa Chama cha upinzani nchini Zimbabwe Tendai Binti |
Katibu
mkuu wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe MDC, Tendai Biti
ameendelea kuvutana na mwenyekiti wake, Morgan Tsvangirai, safari hii
akitaka kiongozi huyo kutoruhusiwa kuwemo wakati wa kikao cha kamati
kuu ya chama kujadili suala la Elton Mangoma.
Mvutano
huo ulianza kushuhudiwa toka juma lililopita punde tu baada ya
tangazo la kamati ya utendaji kutangaza kumsimamisha kwa muda naibu
mweka hazina Elton mangoma kufuatia matamshi yake ya kumtaka kiongozi
wa chama hicho kuachia ngazi.
Lakini
katika kile kinachoonekana kuwa bado kuna mgawanyiko ndani ya chama
hichom hata katibu mkuu wake Tendai Biti anaonekana kutofautiana na
mwenyekiti wake kuhusu kuruhusiwa kushiriki wakati wa mkutano wa
kamati kuu ya chama.
Wachambuzi
wa mambo wameonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa tofauti ndani ya
chama hicho na kwamba kunatoa mwanya kwa chama tawala cha ZANU-PF
kuendelea kujipatia umaarufu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire